loader
Picha

CAG ashukuru Bunge kwa kumpa ushirikiano

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ukaguzi (CAG), Profesa Mussa Assad ameshukuru Bunge kwa kumpa msaada wote muhimu wakati wa kutekeleza majukumu yake. Pia ameshukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kwa kuwa zimekuwa zikisaidia ofisi yake kwa kufanyia kazi ripoti ya ukaguzi na pindi wanapohitaji msaada wao.

Profesa Assad aliyasema hayo wakati wa kufungua Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ambao walikutana kuchagua uongozi wake baada ya uongozi wa awali kumaliza muda wake kikatiba.

Profesa Assad ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, alisema kwa mujibu wa maagizo kutoka kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa baraza la wafanyakazi wa taasisi za umma wanatakiwa kufanya mkutano wa baraza hilo mara mbili kwa mwaka. “Katika ofisi yetu, kwa sababu ya vikwazo vya bajeti, tuliamua kuwa tunakutana angalau mara moja kwa mwaka,” alieleza.

Juzi Baraza hilo lilikutana na kuchagua viongozi wapya na pia kupitisha maazimio ya masuala mbalimbali kwa maslahi ya wafanyakazi. Mkutano ulifanyika ukiwa na kaulimbiu ya: “Ukaguzi Shirikishi, Uwazi na Uwajibikaji ni nyenzo muhimu kuelekea uchumi wa kati.” Baraza hilo lenye wajumbe 110 limejizatiti kutekeleza majukumu yake kwa kuwasaidia wafanyakazi.

“Kwa ujumla Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ina wafanyakazi 957 na kati ya hao wafanyakazi 727 ni wakaguzi na wafanyakazi 230 ambao ni sawa na asilimia 24 ni wafanyakazi wa kada tofauti za idara mbalimbali katika ofisi hiyo,” alifafanua.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Dk Francis Michael ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, alilipongeza kwa kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya CAG ya kuanza taarifa za ukaguzi za kila mwaka.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi