loader
Picha

Jafo: Uchaguzi Serikali za Mitaa utakuwa wa amani

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema anaamini kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu, utakuwa wa amani kwa sababu umekuwa shirikishi.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa 26 jijini hapa, Jafo alisema mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ulianza kwa maandalizi ya kanuni za uchaguzi.

“Kanuni hizi zilianza na wataalamu wetu, wakurugenzi wa halmashauri katika ofisi za serikali za mitaa na baadaye makatibu tawala wa mikoa na baadaye na wakuu wa mikoa, kuandaa kanuni nzuri ambazo katika uchaguzi wa mwaka huu na inawezekana zikawa kanuni za kwanza kutoka kwa utaratibu huu ukilinganisha na chaguzi zilizopita,” alisema.

Alieleza kuwa uchaguzi huo utakuwa wa aina yake kwani katika uchaguzi wa serikali za mitaa inawezekana ni kanuni za kwanza zilizofuata utaratibu wa kukusanya maoni ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau ambalimbali tofauti na chaguzi zingine.

Jafo aliongeza: “Ni imani yangu uchaguzi wa mwaka huu utafanyika kwa amani hasa ukizingatia kuwa umekuwa shirikishi zaidi kwa kushirikisha wadau wote.” Akifafanua zaidi, alisema kanuni hizo zilishirikisha wadau muhimu kwenye uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa vyenye usajili na asasi za kiraia ambazo zilitoa maoni ya kutengeneza kanuni hizo jijini hapa.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiliongoza kwa kupata idadi kubwa ya wenyeviti wa vijiji, vitongozi na mtaa na kufuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo n (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na kufuatiwa na NCCRMageuzi.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi