loader
Picha

Kampuni ya India kutoa bil 15.6/- mradi wa maji

WIZARA ya Maji imesaini mkataba wenye thamani ya Sh bilioni 15.6 na Kampuni ya WAPCOS kutoka India ili kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 29. Akizungumza katika hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba huo, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo alisema mkataba huo ni kwa ajili ya kuandaa taarifa ya kina kuhusu miradi yote ya miji 29.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi jioni jijini hapa, walioshiriki kutia saini mkataba huo wenye sehemu mbili ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo, pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya WAPCOS Ltd, Chandrasekhar Kombathula jijini Dodoma “Mkataba uliosainiwa ni hatua ya awali na inahusu kazi mbili ambazo ni kuandaa taarifa ya kina kuhusu miradi yote ya miji 29 ikiwamo maeneo maji yakapopatikana na ya pili ikiwa ni kuandaa nyaraka za zabuni ili kuwapata wakandarasi watakaotekeleza mradi,” alieleza.

Alisema kazi hiyo inafanyika ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim ya India wenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani milioni 500.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi