loader
Picha

Serikali kutekeleza mfumo rafiki wa biashara, uwekezaji

SERIKALI imeeleza mpango wake wa kusukuma mbele viwanda na kufanya biashara nchini kwa kuhakikisha inatekeleza mfumo rafi ki wa uwekezaji na ufanyaji biashara nchini. Imesema katika kuendeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda serikali itaendelea kuweka vivutio na kufanya maboresho katika maeneo kadha yanayoleta vikwazo ili sekta binafsi ishiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.

“Pamoja na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika viwanda na biashara, utekelezaji wa Blue Print utakuwa tiba ya changamoto zinazotatiza sekta binafsi,” alisema Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake Bungeni jana. Alisema sekta binafsi ni injini ya kujenga uchumi wa viwanda hivyo serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta hiyo inashiriki kikamilifu ujenzi wa uchumi.

Alisema lengo ni kushawishi ujenzi wa viwanda vitakavyo ongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini ili kuondokana na uuzaji wa malighafi nje ya nchi. Aidha, kwa msukumo wa sasa wa serikali, inatarajiwa kwamba sekta binafsi itajenga viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi kwa wingi na vile vinavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na Watanzania walio wengi.

Pia, serikali imesema itaimarisha taasisi zake za viwango na mfumo wa stakabadhi ghalani katika manununuzi, vituo maalumu vya mauzo ili kuwa chachu ya ulinzi wa viwanda na mlaji.

Imesema itaboresha mifumo ya usajili wa biashara na leseni kutoka Brela na pia halmashauri kwa kuhakikisha inatoa mafunzo ya Tehama ili kumudu mfumo wa Dirisha la Taifa la Biashara (NBP) ambao ndio unaotoa leseni za biashara.

Kakunda alisema kwa mwaka 2019/2020 serikali itaendelea na miradi ya kimkakati, urasimishaji wa viwanda na biashara ndogo na za kati, uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na malighafi na kuunganisha masoko.

Alisema ni lengo la serikali kufanya tathmini ya hali halisi ya uzalishaji na mahitaji ya bidhaa viwandani katika viwanda vya sukari, korosho, mafuta ya kula chuma, ngozi nguo na dawa za binadamu.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Na Beda Msimbe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi