loader
Picha

Vifo ajali za bodaboda vyapungua

IDADI ya vifo vya waendesha bodaboda nchini vitokanavyo na ajali imepungua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu kinachoanzia Januari hadi Machi, ikilinganishwa na idadi ya vifo vya bodaboda kwa kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Afande Deusi Sokoni akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu alisema kuwa idadi ya waendeshaji bodaboda waliopoteza maisha kwa mwaka huu ni 73 huku majeruhi wakiwa 121.

Alisema, kwa mwaka jana kwa kipindi kama hicho waliopoteza maisha walikuwa ni 108 huku waliojeruhiwa ni 214. Sokoni aliongeza kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu kwa upande wa waendesha baiskeli waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani walikuwa 23 idadi ambayo ni sawa na ya majeruhi lakini mwaka jana kuanzia Januari hadi Machi, idadi ya waliokufa ilikuwa ni 34 huku waliojeruhiwa wakiwa 30.

Alisema pia waendesha mikokoteni tisa wamekufa na wanne wamejeruhiwa huku mwaka jana aliyekufa alikuwa mmoja na 12 walijeruhiwa. Kundi la watembea kwa miguu ambalo ni moja kati ya waathirika wakubwa wa ajali kwa mwaka huu wamekufa 90 na kujeruhiwa 106.

Wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 163 na kujeruhiwa 179. Kwa upande wa abiria waliokufa kwa ajali kwa mwaka huu ni 108 na 393 wamekumbwa na majeraha mbalimbali wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 191 na majeruhi 575.

TANZANIA imeitaka Dunia na Jumuiya za Kimataifa kutambua kuwa kauli ...

foto
Mwandishi: Na Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi