loader
Picha

Mbinga kupata gari la wagonjwa

MBUNGE wa Mbinga vijijini mkoani Ruvuma, Martin Msuha ameishukuru serikali kwa kutoa kibali cha ununuzi wa magari mawili ikiwemo la wagonjwa kwa Halmashuari ya Wilaya ya Mbinga, ili kusaidia utendaji kazi kwa watumishi na kuhudumia wananchi wa jimbo hilo.

Aidha, amempongeza Rais John Magufuli kutokana na jitihada zake za kukuza na kuharakisha maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mbinga hadi Mbambabay yenye urefu wa kilometa 67 kwa kiwango cha lami.

Msuha alitoa pongezi hizo hivi karibuni wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Mbinga katika sherehe ya kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu iliyofanyika katika viwanja vya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mjini hapa.

Kwa mujibu wa Msuha, mbali na kibali cha magari pamoja na ujenzi wa barabara hiyo, pia serikali imeshatoa Sh milioni 913 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Kigonsera, Sh milioni 100 ili kujenga bwalo katika Sekondari ya Rwanda.

Alisema pia serikali imeshatoa Sh milioni 50 katika Shule ya Sekondari Mateka, Sh milioni 75 kwa Shule ya Wasichana Mbinga na fedha nyingine katika Shule ya Sekondari Kihamili kwa ajili ya kukamilisha mabweni ya wanafunzi.

Aidha, aliwataka wananchi wa Mbinga vijijini kuendelea kushirikiana na serikali yao katika mpango wa kuuza kahawa kupitia vyama vya msingi vya ushirika, badala ya mfumo wa soko huria ambao umesababisha hasara kubwa kwa wakulima wa zao hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye aliwataka wakulima wa kahawa kutoa taarifa sahihi juu ya uwepo wa wanunuzi wa kahawa kwa njia ya magendo.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mbinga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi