loader
Picha

DC atoa siku saba wastaafu ‘walioiba’ pikipiki kurejesha

MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda amempatia siku saba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (DED), Missana Kwangura kuwasilisha polisi majina ya watumishi waliostaafu walioshindwa kukabidhi pikipiki kwa halmashauri hiyo ili wamakatwe na kushtakiwa .

Aidha, amemwagiza Kwangura kuhakikisha katika kikao kijacho cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya anawasilisha hoja zote za mkaguzi wa ndani wa halmshauri hiyo zikiwa zimepatiwa majibu. Mtanda alitoa maagizo hayo jana wakati akiwasilisha kauli ya serikali katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kilichofanyika katika mji mdogo wa Namanyere.

“Wapo watumishi wa halmashauri hii waliostaafu ambapo walikabidhiwa kwa ujumla wao pikipiki nane mali ya halmashauri, wapo waliouziana kwa bei chee, huku wengine wameshindwa kuzirejesha na kuzikabidhi kwa mwajiri wao baada ya kustaafu utumishi wa umma ..., Nampatia DED siku saba awe amewasilisha majina yao polisi ili wakamatwe na pikipiki hizo zirejeshwe halmashauri na kukabidhiwa watendaji wengine katika jitihada ya kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri hii,”alisisitiza.

Alimtaka DED kusimamia maagizo hayo kwa vitendo ndani ya siku saba alizompatia kutekeleza agizo lake hilo. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Sumuni Mwamakula alimhakikishia Mtanda kuwa maagizo yake yatatekelezwa kama alivyoagiza huku akiwataka madiwani kuendelea kusimamia makusanyo ya mapato ya ndani kwa karibu kwa kuwa ndio uhai wa halmashauri hiyo.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Na Peti Siyame

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi