loader
Picha

Ilemela yajenga madarasa 130

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na mbunge wa Ilemela, Dk Angelina Mabula (pichani) pamoja na wananchi wamefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 130 mpaka sasa.

Akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, John Wanga alisema kati ya vyumba hivyo vya madarasa, 24 vipo katika hatua ya kuezekwa, vingine 12 vipo katika hatua ya maboma na vyumba vingine 94 vipo katika hatua ya msingi na kazi za ujenzi bado zinaendelea.

Alisema halmashauri yao ilifanikiwa kupokea Sh milioni 125 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) katika akaunti za shule kwa upande wa elimu ya sekondari na fedha hizo ni kwa ajili ya shule za Nyasaka, Bujingwa, Kisundi, Nyamanoro na Buswelu.

Alisema kila shule imepokea Sh milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa wa vyumba viwili na utengenezaji wa viti na meza 40 kwa kila darasa litakalojengwa.

Kwa upande wake, Diwani wa Buswelu, Sarah Ng’whani alisema ukosefu wa madarasa utakuwa historia katika wilaya yao na aliishuruku Mamlaka ya Majisafi mkoani Mwanza (MWAUWASA) kwa juhudi zao za kuwasaidia katika ujenzi wa vyoo katika shule za msingi na sekondari wilayani Ilemela.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Ilemela

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi