loader
Picha

Kakunda: Kasi ya mauzo yetu nje yameongezeka

WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema kati ya mwaka 2017 na 2018 Tanzania imeendelea kuwa na urari chanya katika mauzo ya bidhaa zake katika nchi za Afrika.

Hayo yamo katika bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyosomwa bungeni jana na Waziri Joseph Kakunda wa wizara hiyo.

Waziri Kakunda alisema Tanzania imeuza zaidi kuliko kununua kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa asilimia 10.63; Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC- kwa asilimia 29.84 na Umoja wa Afrika – AU- kwa asilimia 5.63.

Akifafanua alisema mauzo kwa EAC yalikuwa ni Dola za Marekani milioni 447.5 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 349.6 zilizopatikana mwaka 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.88.

Ongezeko hilo limetokana na mauzo ya bidhaa za chai, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi,mabati, vigae, vyandarua, kemikali, saruji na mafuta ya kupaka.

Tanzania iliagiza kutoka EAC bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 302 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 220.4 kwa mwaka 2017 ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.24.

Akizungumzia SADC alisema mauzo ya Tanzania yalikuwa Dola za Marekani milioni 999.34 mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 877.8 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 12.16.

Aidha, Tanzania iliagiza bidhaa za Dola za Marekani milioni 604.32 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 600.64 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 0.61.

Kwa upande wa Umoja wa Afrika, mauzo ya bidhaa za Tanzania yalikuwa Dola za Marekani milioni 1,485.05 mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola milioni 1,419.84 kwa mwaka 2017 sawa naongezeko la asilimia 4.39.

Ongezeko hilo limetokana na mauzo ya bidhaa za madini, pamba, chai, kahawa, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi, mabati, vigae, vyandarua, kemikali, saruji na mafuta ya kupaka.

Tanzania katika kipindi hicho iliagiza bidhaa za Dola za Marekani milioni 989.01 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 895.88 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.42.

Katika soko la China Tanzania iliongeza mauzo yake kufikia Dola za Marekani milioni 1.98 kutoka dola milioni 142.3 kwa mwaka 2017 hadi kufikia dola milioni 144.28; wakati China iliuza Tanzania bidhaa za Dola za Marekani milioni 356.

Kwa utendaji huo katika soko kuna urari hasi wa biashara wa asilimia 21.79 katika kipindi husika. Katika soko la India mauzo ya Tanzania kwa mwaka 2018 yalikuwa Dola za Marekani milioni 734.27 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 977.6 kwa mwaka 2017.

Tanzania imeagiza kutoka India bidhaa za Dola za Marekani milioni 1,218.07 ikilinganishwa na dola milioni 1,077.60 zilizoagizwa mwaka 2017.

Akizungumzia soko la Japan, Waziri Kakunda alisema Tanzania iliuza bidhaa za Dola za Marekani milioni 66.72 ikilinganishwa na dola milioni 75.7 zilizouzwa mwaka 2017 ikiwa ni sawa na upungufu wa asilimia 13.47 ya mauzo.

Mwaka 2018 Tanzania iliagiza bidhaa za dola za Marekani milioni 398.13 kutoka Japan ikilinganishwa na bidhaa za dola za Marekani milioni 365.2 za mwaka 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 8.27.

Mataifa ya India, Japan na China ndio wafanyabiasha wakubwa na Tanzania.

Pamoja na taifa kuendelea kuongeza kasi ya biashara ya nje, kumekuwepo na changamoto ambazo Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imetaka serikali kuzifanyia kazi.

Jumuiya hiyo imesema kwamba mazingira ya biashara bado sio bora kutokana na utoaji huduma hafifu bandarini, mawasiliano hafifu baina ya mamlaka za Tanzania na wafanyabiashara wa DRC, kuwepo na udanganyifu wa badhi ya wafanyabiahara, mawakala na watumishi wa serikali wasiokuwa waaminifu.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi