loader
Picha

Kuwe na kituo kimoja cha vibali vya biashara-Wabunge

WABUNGE wameiomba serikali iweke kituo kimoja cha utoaji huduma za vibali, ili kupunguza mlolongo na urasimu katika utoaji vibali vya biashara kwa wawekezaji.

Wabunge walitoa ushauri huo wakati wakichangia bajeti ya wizara ya viwanda na Biashara, iliyowasilishwa bungeni hapo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.

Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alisema kuna ukiritimba katika utoaji vibali kwa wawekezaji wanaoanzisha viwanda nchini na ili kuondoa ukiritimba huo kuna haja ya kutolewa vibali hivyo mahali pamoja.

“Taasisi zinazohusika na biashara kama Brela, TFDA, NEMC, TBS na kadhalika zinatakiwa kuwa katika eneo moja ili kurahisisha utaratibu wa utoaji wa vibali kwa wawekezaji wanaokuja nchini,” alisema.

Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM) alisema, kuna kukomoana kwenye biashara na kwamba watu wanapigwa faini zisizostahili huku Waziri wa Viwanda akiwepo.

Aliuliza kazi ya Waziri wa Viwanda ni ipi? “Kila mtu siku hizi amekuwa ni mkusanyaji kodi wakati ingetakiwa kufanywa mahali pamoja. Ninataka kujua maana ya kuwa waziri katika wizara hiyo, naamini ni kukuza biashara, si kuua biashara”.

Kutokana na hilo alimshauri aingilie popote ambako mfanyabiashara anaonewa. Mbunge wa Monduli, Julius Karanga (CCM) alisema hakuna ushirikiano kwenye wizara za serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi