loader
Picha

Wazazi wafundwa

WATAALAMU na wadau wa malezi na makuzi ya mtoto wamehimiza wazazi kuzungumza na kumjengea mtoto upendo na ukaribu tangu akiwa tumboni ili kumuandaa kwa makuzi bora kiakili, kihisia na kimwili.

Kupitia mradi wa Malezi kwa Makuzi ya Mtoto unaotekelezwa na Shirika la kimataifa la Elizabeth Glasser Pediatric AIDS (EGPAF) mkoani Tabora, imeelezwa kwamba tangu akiwa tumboni ambako ndipo ubongo huanzia kukua hivyo ni rahisi kunasa mawasiliano.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na timu ya watendaji wa EGPAF waliotembelea wilayani hapa, wataalamu na wadau wa afya walipongeza mradi huo kuelimisha wazazi na walezi juu ya makuzi yanayozingatia afya na maendeleo ya kisaikolojia hivyo kuwahakikishia watoto haki ya kuishi na kukua.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji Nzega, Mariam Michael alisema mradi umesaidia kwa kiwango kikubwa kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa watoto waliokuwa katika hatari ya kutofikia hatua za makuzi, baada ya wazazi kuelimishwa mbinu mbalimbali.

Alisema chini ya mradi huo unaotekelezwa kwa awamu ya pili kuanzia mwaka jana hadi mwakani, miongoni mwa elimu inayotolewa ni kuhusu wazazi kushiriki malezi ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa kuzungumza na kucheza nao.

“Baadhi ya familia, unaweza kukuta baba na mama wana malumbano tangu mtoto akiwa tumboni na ikamuathiri mtoto anayezaliwa…unakuta mtoto ni mnyonge, hataki kucheza na kuchangamana,”alisema Michael.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi