loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC ataka kodi ilipwe kwa wakati

MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Kissa Kasongwa amewahimiza wananchi kulipa kodi kwa wakati, ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za jamii kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika wilayani humo, Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuna miradi ya huduma za jamii inayojengwa katika Wilaya ya Korogwe ikiwemo Hospitali ya Wilaya, miradi ya barabara, maji, umeme na elimu ambayo yote inategemea kodi ili iweze kukamilika.

“Bado Korogwe kiwango chetu cha kulipa kodi ni kidogo kwani kati ya wananchi 303,000 wa wilaya hii, ni wananchi 2,800 ndiyo wanalipa kodi na tumeshaelekeza kwamba wale wasiokuwemo kwenye mfumo wa TRA ambao mauzo ghafi yao ni chini ya Sh 4,000,000 wanatakiwa kuwa na vitambulisho vya wajasiriamali,” alisema.

Aliwataka wananchi hao watambue kuwa wasipolipa kodi, wanajidhoofisha wenyewe kiamendeleo.

“Hivyo, tujitahidi kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati ili tuweze kutekeleza miradi inayoendelea hapa wilayani kwetu,’’.

Naye, Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao Makuu Salim Beleko, alisema kuwa kodi ni sawa na damu kwenye mwili wa binadamu, hivyo kama serikali itashindwa kupata kodi itashindwa kufanya jambo lolote la maendeleo kwa wananchi wake.

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi