loader
Picha

Simba, Mtibwa Sugar leo ndio leo

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka dimbani kuivaa Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kushinda ili kuendelea kujihakikishia nafasi yao ya kuwa karibu na kutetea taji la ligi hiyo.

Unaweza kuwa ni mchezo wa presha kwa Wekundu hao kwasababu wametoka kupoteza mchezo mmoja na kupata sare moja, tofauti na matarajio yao ya awali hivyo, kwa vyovyote vile hawatakubali kupoteza tena au kupata sare.

Mpaka sasa Simba ina nafasi ya kutetea taji kama tu itashinda michezo minne kati ya mitano iliyobakiza. Inashika nafasi ya pili kwa pointi 82 katika michezo 33 nyuma ya Yanga inayoongoza kwa pointi 83 katika michezo 36m ikiwa imebakiza michezo miwili.

Timu hizo zimekuwa zikipishana katika uongozi wa ligi kwa maana Simba ikishinda leo au kupata sare itarudi katika uongozi kutokana na kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga inaweza kuwa na nafasi ya ubingwa kwa kuwaombea mabaya watani zao wapoteze michezo mitatu na wao washinde waliyobakiza. Simba inakutana na Mtibwa Sugar leo, ambapo mara ya mwisho kukutana Wekundu hao walishinda bao 1-0, Aprili mwaka jana.

Mtibwa Sugar haina cha kupoteza kwani inashika nafasi ya tano kwa pointi 49 katika michezo 35 labda kugombea nne bora.

Iwapo watashinda huenda wakapanda hadi nafasi ya nne na kumshusha KMC, lakini wakipoteza wanaweza kubakia nafasi hiyo.

Lakini hawapo katika mbio za ubingwa, wanaweza kupambana kupata matokeo kwa ajili ya kuweka heshima.

Mtibwa itakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia washambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi ambao muda wote wamekuwa wakipambana bila kukata tamaa ili kufunga.

Safu ya ulinzi ya Simba iko vizuri kwani mpaka sasa imepoteza michezo mitatu tu.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi