loader
Picha

‘Majeruhi wengi upasuaji wa vichwa ni wasiovaa helmeti’

HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesema majeruhi wengi wa ajali wanaofanyiwa upasuaji wa vichwa ni wasiovaa kofi a ngumu (helmeti) pindi wanaposafi ri kwa kutumia pikipiki.

Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo alisema jana kuwa, kutovaa helmeti kuna madhara makubwa kwani miongoni mwa waathirika hao ni waendesha pikipiki wenye kasumba ya mwendokasi na wasiotumia helmeti, pamoja na abiria wao. “Wengi ni vijana kati ya miaka 14 hadi 25 waliomaliza darasa la saba au kidato cha nne na hawa nao, wengi ni ambao hawana mafunzo ya uendeshaji pikipiki yaani anafundishwa leo na rafiki yake mtaani, kesho anaanza kuendesha na kubeba abiria,” alisema Chisseo.

Katika maadhimisho ya hivi karibuni ya Wiki ya Kimataifa ya Usalama Barabarani, Mtandao wa Wadau kutoka Asasi za Ki- raia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera ihusuyo Usalama Barabarani nchini unasisitiza watunga sera na sheria kuifanyia marekebi- sho Sheria ya Usalama Barabarani ya Mwaka 1973 ili itamke kuwa ni lazima kwa dereva wa pikipiki au bajaji na abiria wake kuvaa kofia ngumu wawapo safarini.

Aidha, katika chapisho lake la mapendekezo ya maboresho ya sheria ya usalama barabarani kwa mtazamo wa visababishi vya ajali, Mtandao huo unasema: “Sheria iweke pia kiwango cha ubora wa kofia ngumu ambacho kitatambulika na Shirika la Viwango vya taifa (TBS) kwa kulinganishwa na viwango vya Shirika la Viwango la Kimataifa.”

Mratibu Mradi wa Usalama Barabarani wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Gladness Munuo, anasema utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2015 unaonesha kuwa, matumizi sahihi ya helmeti, hupunguza uwezekano wa vifo itokeapo ajali kwa asilimia 40 na kupunguza uwezekano wa majeraha makubwa kwa asilimia 70.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano huyo wa KCMC, katika kipindi cha miezi sita iliyopita, hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wastani wa majeruhi 14 hadi 15 kwa wiki watokanao na ajali za pikipiki.

“Katika wodi ya mifupa kunakofanyika pia upasuaji wa miguu, mikono au kichwa, kwa wiki tunakuwa na wastani wa majeruhi 15 hadi 30 ingawa idadi hiyo nayo inazidi kupungua, lakini wengi kati ya 6 hadi 7 ni wale wanaopata madhara makubwa katika vichwa wanapopata ajali wakiwa kwenye pikipiki kutokana na kutovaa helmeti,” alisema.

Akaongeza: “Tatizo au kisababishi kikubwa cha hali hii ni wengi kutovaa helmeti sasa ikitokea ajali akiwa kwenye pikipiki, anagonga kichwa kwenye lami; au kama amevaa bila kufunga, ikitokea ajali, kofia inatoka kabla yeye hajafika chini, akifika anagonga kichwa moja kwa moja kwenye lami, jiwe au sehemu ngumu…”

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi