loader
Picha

Simba yachanja mbuga

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamezidi kukaribia kutetea ubingwa wao baada ya jana kuitandika Mtibwa Sugar kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 85 baada ya kucheza michezo 34 na kuishusha Yanga kileleni, ambayo ina pointi 83 na imeshacheza mechi 36 na kubakisha mechi mbili kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.

Simba sasa imebakisha pointi tano tu katika mechi nne ilizobakiza ili iweze kutangazwa bingwa, kwani itafikisha pointi 90 wakati Yanga hata kama watash- inda mechi zake mbili zilizobaki, itaishia kufikisha pointi 88.

Katika mchezo huo wa jana, Meddie Kagere ameen- delea kuongeza akaunti yake ya mabao baada ya kuifungia Simba bao la kwanza katika dakika ya 32 na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Kagere sasa ana mabao 21 na kuzidi kuongoza katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akimuacha Heritier Makambo wa Yanga katika nafasi ya pili akiwa na mabao 16 sawa na Salim Aiyee wa Mwadui mwenye idadi kama hiyo.

Simba iliendeleza makali yake ilipoandika bao la pili katika dakika ya 47 lililofungwa na Clatous Chama baada ya kupiga shuti kali nje ya meya 18 baada ya kipa wa Mtibwa kuutokea mpira nje ya 18. Emmanuel Okwi aliikamilishia Simba ushindi baada ya kufunga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jonas Mkude.

Katika dakika ya tisa na 22, Chama na Kagere nusura waifungie Simba mabao lakini hawakuwa makini na licha ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga, kipa wa Mtibwa Sugar aliokoa hatari hizo. Yanga juzi ilishika uon- gozi huo wa ligi baada ya kuifunga Ruvu Shooting ya Mlandizi, Pwani kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru huku bao hilo pekee likifungwa na Mcongo Tshishimbi.

Vikosi Simba: Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tsha- balal’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni Jonas Mkude, Clatous Chama, Haruna Niyonzima/ Hassan Dilunga dk81, John Bocco/Muzamil Yassin dk60, Meddie Kagere/Adam Salamba dk73 na Emmanuel Okwi.

Mtibwa Sugar; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Shabaan Nditi, Salum Kihimbwa/Salum Kihimbwa dk83, Ally Makarani, Jaffar Kibaya/Saleh Khamis dk70, Riphat Msuya na Haroun Chanogo/Ismail Aidan dk62. Wakati huohuo, Stand United ya Shinyanga wameifunga Kagera Sugar kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

MWANAMUZIKI mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro ‘Wana Njenje’, Mabrouk Hamis ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi