loader
Picha

TOC wamuunga mkono JPM

SIKU ya Olimpiki Duniani itafanyika kitaifa Chato mkoani Geita mwaka huu ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Dk John Magufuli, imeelezwa. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanza- nia (TOC), Filbert Bayi, Siku ya Olimpiki kitaifa itafanyika Chato Juni 23, mwaka huu.

Bayi alisema Dar es Salaam jana kuwa, TOC imeamua kupeleka siku hiyo Chato ili kuunga mkono jitihada za Magufuli anazofanya za kuendeleza nchi tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Alisema tangu aingie madarakani, Magufuli amekuwa akipiga vita ubadhirifu, ufisadi na ubabaishaji wa kila aina ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kuiwezesha kuelekea katika uchumi wa kati.

Alisema pia katika michezo, Serikali ya Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi inapiga hatua katika michezo mbalimbali, ikiwemo kujenga uwanja mkubwa wa kisasa Makao Makuu ya nchi Dodoma. Chato ni moja ya wilaya zilizopo katika mkoa wa Geita na ni mahali ambako alizaliwa Rais Magufuli.

Siku ya Olimpiki hufanyika kila mwaka katika tarehe tofauti tofauti na imekuwa ikisherehekewa kwa kucheza michezo mbalimbali, ambapo kwa Tanzania utachezwa mchezo wa riadha kwa wanafunzi na watu mbalimbali.

Katika siku hiyo, watoto wadogo na wazee watashiriki mbio za kilometa 2.5 wakati wanafunzi na watu wengine, watakimbia katika mbio za kilometa, ambapo mshiriki mwenye umri mdogo zaidi na yule mwenye umri mkubwa zaidi, watapewa zawadi za fedha taslimu. Tayari mikoa ya Mbeya, Singida, Kagera, Dar es Salaam, Pwani, Mwanza na Mara imeshawahi kuwa wenyeji wa siku hiyo ya Olimpiki katika miaka tofauti tofauti.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi