loader
Picha

WB yatoa mil 77/- za miradi ya ufanisi

KATIKA kuboresha huduma za maji, Benki ya Dunia (WB) imeipa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Sh milioni 77 ikiwa ni malipo ya miradi ya ufanisi.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Rebman Ganshonga wakati wa kikao cha baraza la Madiwani kupitia taarifa za Kata. Alisema kuwa kwenye bajeti iliyopita Halmashauri ilipokea Sh milioni 33 ikiwa sehemu ya mradi wa malipo ya ufanisi katika miradi ya maji na kuongeza kuwa fedha hizo zimelenga katika kufungua vituo vipya vya kutoa huduma ya maji katika Kata ya Dutumi, Kikongo na katika kata nyingine za halmashauri ya wilaya ya Kibaha vijijini.

“Tumefanya vizuri katika miradi ya malipo kwa ufanisi ndiyo sababu ya kuongezewa fedha ambazo zitasaidi uboreshaji huduma za maji,”alisema Ganshonga. Alisema licha ya baadhi ya changamoto za huduma za maji, halmashauri imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Diwani wa Kata ya Dutumi, Mkali Kanusu alisema Kata yake imepokea Sh milioni 13 kwa ya malipo ya ufanisi na kwamba wamezitumia fedha hizo katika uboreshaji miundombinu ya maji. Kanusu alisema wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya maji ikifika katika msimu wa kiangazi kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika chanzo wanachokitegemea kwenye Mto Ruvu.

Alisema wanaipongeza Benki ya Dunia kwa kuwapatia fedha hizo kwani itawasaidia kukabili changamoto ya maji. “Lengo ni kuhakikisha maji yanapatikana kwa uhakika na wananchi wanaondokana na adha hiyo,”alisema Kanusu.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: John Gagarini,Kibaha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi