loader
Picha

Mwakilishi wa Kuteuliwa ataka ACT kuchunguzwa

MWAKILISHI wa kuteuliwa na Rais Said Soud amemtaka Msajili wa vyama vya siasa kukichunguza chama cha ACT-Wazalendo ambacho kinaonekana viongozi wake kwenda kinyume na masharti ya sheria ya vyama vya siasa nchini kwa kufanya shughuli zake na kuhusisha imani za kidini.

Soud alisema hayo wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2019- 2020. Alisema viongozi wa chama hicho kwa nyakati tofauti wameonekana wakifanya shughuli za kisiasa kwa kuhusisha imani za dini.

Soud alisema kwa mujibu wa masharti ya msajili wa vyama vya siasa ni marufuku viongozi wa vyama kufanya kazi zao za kisiasa kwa kuashiria muelekeo wa kidini. “Spika tunamuomba msajili wa vyama vya siasa nchini kukichunguza chama cha ACT-Wazalendo ambapo hivi karibuni viongozi wake walionekana wakifanya shughuli za kisiasa kwa kuingiza masuala ya imani za kidini,”alisema.

Alisema sheria ya msajili imepiga marufuku vyama vya siasa na viongozi wake katika utekelezaji wa majukumu yao kuhusisha imani za dini. Soud alisema kama msajili wa vyama vya siasa atayapuuza matukio kama hayo ambayo ni hatari na yanaweza kuligawa taifa katika misingi ya imani ya dini.

“Spika namuomba msajili wa vyama vya siasa ambaye majukumu yake yanafanya kazi katika Jamhuri ya Muungano kukichunguza chama hicho na matukio hayo yanayohatarisha kuligawa taifa katika misingi ya imani ya dini,”alisema. Hivi karibuni viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo walionekana wakipandisha bendera baadhi ya maeneo ya vijijini huku wakisoma Kuran pamoja na kufanya ibada ya dhikri.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi