loader
Picha

SMZ, Unesco kuzungumzia ukanda wa biashara Darajani

UJUMBE wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) unatazamiwa kufanya ziara makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa, Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO), nchini Ufaransa kwa ajili ya kuzungumza suala la ujenzi wa mradi wa Ukanda wa biashara wa Darajani ambao utahusisha ujenzi wa maduka ya biashara.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum (SMZ), Haji Omar Kheri wakati akifanya majumuisho ya michango ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia bajeti hiyo kwa mwaka wa 2019-2020. Kheri alisema kwa mujibu wa masharti ya miji iliyopo katika urithi wa majengo ya kale, ujenzi wake au marekebisho yanahitajika kwanza kupata baraka kutoka kwa Unesco.

Alisema serikali inakusudia kulitumia eneo la darajani kuwa ni ukanda wa biashara kwa ajili ya kujenga maduka ya biashara. Kheri alisema hadi sasa ujenzi wa eneo hilo umesisimishwa kwa sababu ya kushindwa kupata kibali kutoka Unesco ambao ndiyo wenye dhamana ya kushughulikia majengo ya kale.

“Spika napenda kuliarifu Baraza la Wawakilishi kwamba ujenzi wa eneo la ukanda wa biashara Darajani kwa sasa umesitishwa hadi hapo tutakapopata kibali kutoka Unesco,”alisema. Kheri alisema ujenzi wa maduka ya biashara wa Darajani ni muhimu kwa ajili ya kuwaendeleza wananchi kuzitumia fursa za kibiashara.

Aidha alisema ujenzi wa maduka ya kisasa katika ukanda huo kwa kiasi kikubwa utaufanya mji wa Zanzibar kuwa na harakati za kibiashara na kutoa nafasi kwa wananchi mbalimbali kufanya shughuli za biashara ikiwemo wanaotoka nje ya Zanzibar.

“Hizo ndiyo sababu zilizotufanya kulitumia eneo la Darajani kwa ajili ya shughuli za kibiashara ikiwemo ujenzi wa maduka ambao utawaneemesha wafanyabiashara kupiga hatua kubwa za kibiashara,”alisema. Mji wa Zanzibar uliopo katika ukanda wa Mji Mkongwe unatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (Unesco) na kuingizwa katika urithi wa kimataifa kutokana na kuwa na majengo ya kale yaliyobeba historia muhimu ikiwemo ya biashara ya utumwa.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi