loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Taarifa Tume Haki za Binadamu hazijazuiwa kujadiliwa’

IMEELEZWA kuwa hakuna sheria yoyote inayokataza taarifa za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kujadiliwa Bungeni endapo mbunge ataona kuna jambo la kuibua kutoka kwenye taarifa iliyoibuliwa.

Akijibu swali la mbunge wa Mgogoni Dk Suleiman Ally Yusuf (CUF), kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha alisema kwamba tume imekuwa ikitimiza wajibu wake na ripoti zake ziwazi. Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alikuwa anataka kujua kwa nini ripoti za tume hiyo haziwekwi wazi kwa umma na kama serikali haioni kuwa wakati umefika kujenga utamaduni wa ripoti hizo kujadiliwa bungeni.

Naibu waziri huyo alisema kwamba ni kweli kuwa ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ikisomwa kwa pamona na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina ipa tume mamlaka ya kufanya uchunguzi wa uvunjikwaji wa haki za binadamu na baada ya uchunguzi kubaini ripoti zitapelekwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji wa maoni ya tume.

Aidha sheria inataka tume kuwasilisha taarifa yake ya mwaka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Mawaziri kupitia kwa mawaziri wanaoshughulikia masuala ya haki za binadamu Tanzania bara na visiwani.

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi