loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuongeze nguvu kudhibiti dengue

TAARIFA za serikali na taasisi za afya za ongezeko la wagonjwa wa homa ya dengue nchini zinadhihirisha wazi kuwa, tunapaswa kuongeza nguvu kudhibiti ugonjwa huo.

Kama ilivyo magonjwa mengine ya mlipuko, dengue imesababisha watu zaidi ya 1900 kuathirika nao nchini huku baadhi wakipoteza maisha ama kwa kuchelewa tiba au kwa kutogundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hali katika Mkoa wa Dar es Salaam ni mbaya zaidi, kwani zaidi ya asilimia 90 ya waathirika ni wakazi wa mkoa huo.

Ingawa tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali, ikiwemo kutoa elimu, kuongeza vituo vya afya vya serikali kutoa vipimo na matibabu ya ugonjwa huo, kuweka wazi ukubwa wa tatizo kwa kueleza dalili, walioathirika na namna ya kujikinga, bado naona kuna nguvu ya pamoja inahitajika zaidi kukabiliana na tatizo hili. Afya ni sekta muhimu kwa mustakabali wa taifa lolote.

Rais Magufuli aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, taifa la watu wasio na afya haliwezi kupata maendeleo.

Kauli hiyo na nyingine nyingi za viongozi wa serikali wakiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na naibu wake, Dk Faustine Ndugulile na viongozi wa dini na wa kijamii, inaongeza nguvu katika kile ninachomaanisha kuwa, nguvu ya pamoja inaweza kudhiti tatizo hili.

Nguvu hiyo ninapaswa kuanzia katika ngazi ya familia, wazazi na walezi wazungumze katika familia zao kuhusu tatizo la homa hii, dalili zake na namna ya kujikinga na kisha wachukue hatua kuondoa kila mazingira hatarishi ikiwemo kufukia madimbwi ya maji yanayosababisha mazalia ya mbu.

Tayari Jiji la Dar es Salaam limeanza jitihada za udhibiti mbu kwa kunyunyizia dawa ya viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu waenenezao ugonjwa huo lakini hatupaswi kusubiri serikali itufanyie kila kitu ni lazima nasi tuchukue hatua inayowezekana kuchukuliwa ndani ya uwezo wetu.

Hata kwa mikoa na maeneo ambako ugonjwa huu haujaripotiwa, tuudhibiti kwa kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha paa la nyumba na kutoruhusu maji kutauama au kuwa wazi hata kama ni maji safi na salama.

KATIKA miaka ya karibuni msimu wa mavuno kumekuwa na watu ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi