loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gavana BoT awashukia wahasibu kuzagaa fedha haramu mitaani

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu kote nchini kuhakikisha wanazingatia maadili ya kazi yao, ikiwa ni - tumizi ya fedha haramu, ukwepaji kodi na malipo hewa ili kulinda taaluma yao na uchumi wa Taifa.

Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) unaoendelea jijini hapa. Profesa Luoga alisema kwa kufanya hivyo, kutaongeza imani ya Watanzania kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu. Aliongeza kuwa endapo watafuata utaratibu huo, itasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu hapa nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno alisema kuwa lengo la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu. Aliongeza kuwa katika mkutano huo, mada 11 zitawasilishwa na kujadiliwa zikiwemo za Fedha,Tehama, Uadilifu na Muongozo wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu kuhusiana na Fedha Haramu na Kanuni za Nidhamu.

“Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini imeendelea kuwaelimisha wahasibu na wakaguzi wa mahesabu juu ya kufanya kazi kwa kuzingatia wajibu na weledi pindi watekelezapo majukumumu yao ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote wanaokiuka maadili,” alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Alisema bodi yake imetunga mwongozo ulioanza kutumika Aprili Mosi, mwaka huu kwa wafanyabiashara ndogo kuhakikisha kuwa wanakagua hesabu zao, lengo likiwa ni kuongeza kodi na Mei Mosi, mwaka huu, umeanza kutumika Mwongozo wa Fedha Haramu na Juni 15, mwaka huu zitaanza kutumika Kanuni za Uadilifu.

Akizungumzia mkutano mkuu huo wa mwaka, alisema unashirikisha watu 300 ambao ni wahasibu na wakaguzi wa hesabu kutoka taasisi na mashirika mbalimbali, maofisa kutoka BoT na benki nyinginezo, wataalamu wa fedha na taasisi za bima.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi