loader
Picha

Mabingwa Simba, Sevilla kuchuana leo

MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL), Simba leo wanashuka uwanjani katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ Sevilla utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kimataifa umeandaliwa na wadhamini wa Simba, ikiwa ni sehemu ya kutangaza soka la Tanzania Kimataifa kupitia timu hiyo iliyowahi kutwaa mataji mengi Ulaya. Katika historia ya soka la Tanzania kwa miaka ya karibuni huo ni mchezo wa kwanza mkubwa wa kimataifa kwa timu za Ulaya kucheza na klabu ya hapa nchini. Everton ya Ligi Kuu England iliwahi kuja lakini ilicheza na Gor Mahia ya Kenya.

Ni mchezo mzuri kwa wekundu hao kujipima na kutathmini kikosi chao kuelekea mwishoni mwa msimu wakiwa na furaha ya kunyakua taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Sevilla ni timu yenye historia katika Ligi ya Ulaya ikinyakua mataji matano katika msimu wa 2005/2006, 2006/2007, 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016. Pia, iliwahi kutwaa taji la Uefa Super Cup mwaka 2006.

Kwenye La Liga wana miaka mingi hawajachukua Kombe na inaonekana walichukua mara moja tu msimu wa mwaka 1945/1946. Msimu huu timu hiyo imemaliza ligi katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 59 sawa na Getafe inayoshika nafasi ya tano, huku vigogo Barcelona wakiongoza kwa pointi 87, wakifuatiwa na Atletico Madrid pointi 76, Real Madrid 68 na Valencia 61.

Kwa nafasi waliyopo msimu ujao wana nafasi ya kucheza tena ligi ya Europa hivyo, ni mechi nzuri itakayokuwa na mvuto pande zote mbili, kwa kuwa Simba ina uzoefu wa mechi za kimataifa baada ya kushiriki michuano ya Afrika.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi