loader
Picha

Wataka sera kulazimisha wageni kuajiri Watanzania

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameitaka serikali kutayarisha sera ya ajira itakayokuwa mwongozo na kuwabana wawekezaji wa kigeni, kuwalazimisha kuajiri wafanyakazi wazalendo nchini katika miradi ya vitega uchumi.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa jimbo la Shaurimoyo, Hamza Hassan Juma wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka wa fedha 2019/20. Juma alisema hadi sasa hakuna sera ya ajira ambayo itawaelekeza wawekezaji wa nje kuajiri wafanyakazi wazalendo katika sekta mbalimbali, ikiwemo hoteli za kitalii.

Alisema ni kweli hoteli nyingi za kitalii zimeajiri wafanyakazi wa kigeni kwa visingizio mbalimbali, ikiwemo hakuna wafanyakazi wazalendo wenye sifa katika idara mbalimbali. ‘’Tunapiga kelele sana katika suala la ajira kwa wafanyakazi wetu wazalendo katika sekta za hoteli za kitalii...njia pekee ya kudhibiti na kukabiliana na tatizo hilo ni kutunga sera itakayowabana wawekezaji hao kuajiri wafanyakazi wa wazalendo,’’ alisema.

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma akichangia bajeti hiyo alisema ni kweli wapo wawekezaji wengi wa nje hawatoi kipaumbele cha ajira kwa wafanyakazi wazalendo. Alisema njia pekee ya kuwabana wawekezaji wa aina hiyo ni kuweka sheria madhubuti na kuhakikisha wafanyakazi wazalendo wanapata ajira katika sekta mbalimbali.

Alisema zipo baadhi ya nchi wakati mwekezaji anapokwenda kuwekeza anapewa masharti, ikiwemo kuhakikisha asilimia fulani ya ajira inakwenda kwa wananchi wa sehemu ile. ‘’Sasa wakati umefika tuhakikishe kwamba tunatunga sera zitakazowabana wawekezaji wanaokuja kuwekeza kutoa ajira kwa wafanyakazi wazalendo ili wafaidike na sekta ya uwekezaji,’’ alisema.

Naye, mwakilishi wa jimbo la Chaani, Nadir Abdulatif Yussuf aliwapongeza wawekezaji wazalendo wakiongozwa na Mwenyekiti wa makampuni ya Azam, Said Salim Bahressa kwa kutoa nafasi nyingi za ajira kwa wafanyakazi wazalendo katika vitenga uchumi vyao nchini.

Alisema Bakhresa ameajiri sehemu kubwa ya wafanyakazi kutoka Zanzibar katika vitega uchumi vyake, hivyo wazalendo kufaidika na uwekezaji wake. ‘’Wawekezaji nchini waige mfano wa mwekezaji mzalendo Bakhresa kwa kutoa ajira sehemu kubwa kwa wananchi kutoka Zanzibar, hivyo kufaidika na uwekezaji wake,’’ alisema.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi