loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Marekebisho sheria ya wanyama kuanza kutumika Julai mosi

MAREKEBISHO ya Kanuni ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama yataanza kutumika Julai mosi, mwaka huu, ili kuwadhibiti watendaji waliokuwa wakitumia kisingizio cha sheria na kuwanyima haki wanyama.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, alisema hayo jana bungeni na kuongeza kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa wakiona wanyama kama wahalifu wakati ni viumbe hai wenye haki zao.

Mpina alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Immaculate Semesi (Chadema) aliyehoji ikiwa serikali haioni kama kumekuwa na ukiukwaji wa haki za wanyama wakati wanyama wanapokamatwa na kushikiliwa na watendaji.

Akijibu swali hilo, Waziri Mpina alikiri kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa wakikiuka haki za wanyama na kuwachukulia wanyama kama wahalifu wakati Sheria ya Ustawi wa Wanyama inasema wanyama wanapokamatwa wanatakiwa kupewa maji, kulisha na kutazamwa.

“Tumeboresha Kanuni ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama na itaanza kutekelezwa Julai mosi, ili watendaji wanaonyanyasa wanyama kwa kisingizio cha kutekeleza sheria wadhibitiwe. Watanzania lazima wafahamu mifugo ni rasilimali ya nchi nzuri,” alisema.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema serikali imeanza kufanyia kazi teknolojia ya utambuzi wa wanyama na watakuwa wakivalishwa herini badala ya kuwatambua kwa kuwachoma ili kuwaweka alama. Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga(CCM) aliyebainisha kuwa utaratibu wa kuwatambua wanyama kwa kuwapiga chapa kwa kuwachoma ni wa kikatili.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi