loader
Picha

‘Kuzuiwa mifuko ya plastiki kutaongezea kipato Watanzania’

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba amesema Watanzania wengi watapata kipato kwa kutengeneza, kuuza na kusambaza mifuko mbadala baada ya zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni mosi, mwaka huu.

Alisema mbali ya kipato hatua hiyo pia itawezesha wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani ya nchi kuanzisha viwanda vidogo vya kutengeneza mifuko mbadala, hatua itakayokuza uchumi na kuzalisha ajira.

Aliyasema hayo juzi alipokutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam. Alisema zaidi ya nchi 60 tayari zimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya aina hiyo na maisha yanakwenda vizuri bila uharibifu wa mazingira.

Aliwataka Watanzania wawe na mtazamo chanya wa zuio hilo na kusema kwamba ilipita miaka 30 baada ya Uhuru mifuko ya plastiki kuanza kutumika nchini na maisha yalikwenda vizuri.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara alisema serikali imejipanga kusimamia marufuku hiyo ya matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

Alisema pia maandalizi yamefanywa kupeleka elimu juu ya jambo hilo kupitia shule za msingi, sekondari na kwenye mikusanyiko ya ibada. “Kila liliko kusanyiko la ibada tutawaomba viongozi tutoe elimu juu ya zuio hili ili wananchi washirikiane na serikali,” alisema.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka, alisema baraza litatumia kanda zake saba kuhakikisha utekelezaji wa zuio hilo unakwenda vizuri kwa kushirikiana na mikoa kuandaa maeneo ya kuhifadhi masalia ya mifuko baada ya zuio.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi