loader
Picha

Polisi yamshikilia mwanafunzi aliyempa mimba mwenzake

POLISI wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa inamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kirando mwambao mwa Ziwa Tanganyika, Venance Kasolo(17) kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake anayesoma kidato cha kwanza shuleni hapo.

Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi wilayani Nkasi, imethibitisha kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa juzi saa 5:00 asubuhi akiwa darasani shuleni hapo na kufikishwa katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kata ya Kirando. Kwa masharti ya kutoandikwa majina yake gazetini kwa kuwa sio msemaji wa jeshi la polisi, askari kutoka Kituo kikuu cha Polisi kilichopo katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi alisema kuwa mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa shauri lake kukamilika.

“Alipohojiwa mwanafunzi huyo, alikiri kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wanayesoma pamoja katika Shule ya Sekondari Kirando, akidai kuwa wamefanya tendo la ndoa mara nne,” alisema mtoa taarifa.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kirando, Godwin Ndalama alikiri kuwa uongozi wa shule yake haukufahamu lolote kuhusu tuhuma za mwanafunzi huyo kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake, mpaka pale alipokamatwa na polisi na kufikishwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano. Akizungumzia mkasa huo, Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (Sekondari), John Lupenza alikiri kutokea kwa mkasa huo.

Alisema tayari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Missana Kwangura ametaarifiwa huku akimuagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Kirando, Ereneo Mgina kumwasilishia taarifa ya mkasa huo kwa kina na kwa maandishi haraka iwezekanavyo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Nkasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi