loader
Picha

Uingereza yajipanga na uchaguzi mpya baada ya May kungátuka

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Theresa May ametangaza atangátuka madarakani kwenye uongozi wa chama cha kihafidhina cha Conservative na kutoa mwanya kwa taifa hilo kuchagua kiongozi mwingine.

May ameeleza leo, Ijumaa, kuwa amefanya kila awezalo kufanikisha mpango wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (BREXIT) huku akielezea kwa masikitiko kuwa ameshindwa kukamilisha kazi hiyo. Hata hivyo, May ataendelea kushikilia uongozi wa Conservative hadi pale uchaguzi mpya utakaopofanyika ili kumpata mrithi wake.

Chama hicho kinatarajiwa kupata kiongozi mpya kabla ya mwishoni mwa Julai. Kwa mujibu wa BBC, May atakuwa bado madarakani wakati Rais wa Marekani, Donald Trump atakapoitembelea Uingereza mwishoni mwa Juni, mwaka huu.

MAHOJIANO yenye lengo la kuamua mustakabali wa uwepo madarakani wa ...

foto
Mwandishi: BBC

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi