loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi 3,000 wapoteza udahili

WANAFUNZI zaidi ya 3,000 kutoka vyuo mbalimbali nchini Kenya wamepoteza udahili katika vyuo vyao kutokana na hatua ya serikali ya kufuta alama ya ufaulu ya daraja D+ kutoka katika madaraja ya ufaulu wa mitihani ya vyuo. Hatua hiyo, ilichukuliwa na Waziri wa Elimu wa Kenya, Belio Kipsang’ katika barua iliyotumwa kwa wakurugenzi wanane wa elimu nchini.

Katika barua hiyo, waziri huyo aliwaagiza kuhakikisha kuwa katika vyuo vya serikali na vya binafsi vinafundisha wanafunzi waliopata angalau daraja la wastani tu. Waziri huyo alisema daraja la mwisho la ufaulu litakuwa daraja la ‘C’ na halitakuwa daraja la ‘D’ kama ilivyokuwa kipindi kilichopita. Kwa mwanafunzi anayetaka kwenda kusoma katika ngazi ya cheti atalazimika kupata alama ‘C’ ambayo itakuwa ndio daraja la mwisho la ufaulu. Kwa upande wa mwanafunzi anayetaka kwenda kusoma ngazi ya astashahada atalazimika kupata ufaulu wa daraja la (P1) na ‘C+’.

Sababu za serikali za kufuta daraja hilo kwa mujibu wa waziri ni kulinda hadhi ya elimu nchini humo. “Wakuu wote wa vyuo vya umma na binafsi mnataarifiwa kuwa kipimo cha alama ya kujiunga na Mafunzo ya Chuo cha Ualimu (TTC) kitabaki kuwa kama kilivyoelezwa katika sheria namba 50 ya mwaka 2016,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Mwaka jana aliyekuwa Waziri wa Elimu, Amina Mohamed alibadilisha viwango vya madaraja ya kujiunga na vyuo vya ualimu kutoka alama C ikiwa ni alama ya ufaulu wa mwisho na kuishusha hadi alama D+. Hatua hiyo ilikumbana na vikwazo na upinzani kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu. Chama cha Walimu (TSC) kilipinga hatua hiyo kikiungwa mkono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi