loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Hatukujua kuwa Rais Museveni anafanya kampeni’

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC), Jaji Simon Byabakama (pichani) amesema tume hiyo haikuwa na taarifa kuwa Rais Yoweri Museveni anafanya kampeni za chinichini kabla ya muda wa kampeni ambao ni mwakani.

Jaji Byabakama aliyasema hayo wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika makao makuu ya tume hiyo Mjini Kampala. Kauli hiyo ilikuja baada ya viongozi wa upinzani kufikisha malalamiko yao katika tume hiyo kuwa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika anafanya kampeni za chini chini kupitia chama chake cha NRM.

Kutokana na hali hiyo, tume hiyo ilimtaka Rais Museveni kuacha kufanya kampeni za chinichini kwa sababu bado mwaka mmoja na nusu kufika wakati wa kufanya kampeni. Viongozi wa upinzani wakiongozwa na kiongozi wa chama cha FDC, Dk Kizza Besigye alisema wamekuwa wakiandamwa na jeshi la polisi kutokana na kufanya mikusanyiko midogo wakituhumiwa kufanya kampeni za kisiasa.

Walihoji iweje wao wakikusanyika wanashughulikiwa kwa madai kuwa wanafanya mambo ya siasa, lakini wamekuwa wakimuangalia Rais Museveni akifanya mikutano ya kisiasa na kuitumia kufanya kampeni bila kukemewa. Tayari Rais Museveni ndiye mgombea pekee katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021 kupitia chama chake cha NRM.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi