loader
Picha

Kufungiwa Huawei kuathiri wateja

HATUA ya Marekani kufungia kampuni ya Huawei kushirikiana na kampuni zake imeshutumiwa kwamba itaathiri mabilioni ya wateja. Aidha, kampuni hiyo inaendelea na mchakato wa kufungua mashitaka dhidi ya serikali ya Marekani kutokana na hatua ya kuizuia.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwanasheria wa kampuni hiyo ya Huawei, Song Liuping alisema zuio hilo la biashara pia litaleta madhara kwa kampuni za Marekani na wakati huohuo kuathiri ajira. Hivi karibuni Marekani ili- iweka Huawei kwenye orodha ya kampuni ambazo kampuni za Marekani haziwezi kufanya nazo biashara isipokuwa ziwe na leseni.

Huawei ambayo ni kampuni ya China ni kinara wa dunia wa utengenezaji wa vifaa vya mawasiliano. Kwa mujibu wa Marekani, zuio hilo limezinga- tia usalama wa taifa. Kampuni hiyo imekuwa ikikanusha madai ya kutumia bidhaa zake kuhatarisha usalama, huku ikisisitiza kuwa haiko chini ya serikali ya China.

Song alisema uamuzi huu unatishia na kuathiri wateja katika nchi zaidi ya 170 wakiwamo zaidi ya wateja bilioni tatu wanaotumia bidhaa na huduma za Huawei duniani. “Kwa kuzuia kampuni za Marekani kufanya biashara na Huawei, moja kwa moja serikali itaathiri zaidi ya kampuni 1,200 za Marekani. Hii itaathiri pia maelfu ya ajira za Wamarekani,” alisema.

Kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Marekani kuiorodhesha Huawei katika kampuni ambazo ni marufuku kwa kampuni zake kushirikiana nayo isipokuwa kwa kibali, kampuni ya Google ilipiga marufuku Huawei kutumia baadhi ya huduma kutoka mfumo wa uimarishaji kazi ya simu, Android.

Kutokana na marufuku hiyo, aina mpya za simu za Huawei hazitaweza kutumia baadhi ya programu kutoka Google apps. Huawei ambayo ni kampuni ya pili kubwa duniani, imesema itaendelea kutoa mfumo wa kuimarisha matumizi ya simu zake na huduma za baada ya mauzo ya bidhaa zote za simu ambazo zimeshauzwa na zinazosubiri kuuzwa duniani. Mvutano huu umetajwa kuwa utakuwa na athari kwa wateja wa bidhaa za Huawei hususani Afrika.

MAHOJIANO yenye lengo la kuamua mustakabali wa uwepo madarakani wa ...

foto
Mwandishi: HONG KONG, China

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi