loader
Picha

Tanzania yaweka rekodi mapato ya madini

TANZANIA imeweka rekodi ya dunia kwa ukusanyaji wa mapato, yatokanayo na sekta ya uchimbaji wa madini, hatua inayotokana na usimamizi mzuri wa rasilimali hiyo, ikichangiwa na mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na serikali katika sekta hiyo hivi karibuni.

Hayo yalielezwa jana na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbas katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisisitiza kuwa hatua hiyo, imetokana na utendaji kazi wa ‘kisayansi’ wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli. Dk Abbas alisema katika kipindi cha miezi 11 kuanzia Julai, 2018 hadi juzi, serikali imeweza kuingiza Sh bilioni 302.63 za mapato hayo, ikiwa imesalia mwezi mmoja mwaka kukamilika.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2017 na 2018, kiasi cha Sh bilioni 301 za mapato hayo zilikusanywa ikiwa ni pungufu kwa wastani wa Sh bilioni moja zilizopatikana hadi sasa kwa mwaka huu unaoishia Juni.

Aidha, alisema mwaka 2015/2016 kiasi cha Sh bilioni 210 zilipatikana kwa kipindi hicho ikilinganishwa na Sh bilioni 302 za msimu huu, suala alilosema kuwa kwa kiasi kikubwa limeonesha mafanikio katika sekta hiyo. Alisema kukusanywa kwa kiasi hicho cha fedha, kabla ya hata kukamilika kwa mwaka, kunatokana na usimamizi mzuri wa serikali katika sekta hiyo muhimu, ulioendana na kuanzishwa kwa masoko ya madini, miezi mitano tangu Rais Magufuli aagize uanzishwaji wake.

Alisema hadi sasa kuna jumla ya masoko 24 ya madini, yaliyoanzishwa ndani ya kipindi cha miezi mitano, ambayo kimsingi yameonekana kufanya vyema katika ukusanyaji wa mapato hatua inayotoa matumaini.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi