loader
Picha

Simba iliniumiza kichwa- Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ni miongoni mwa makocha waliokataa kuipongeza Simba ilipotwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini ameivulia kofia kuwa ni moja ya timu iliyomuumiza kichwa msimu huu.

Baada ya kumalizika kwa mechi ya mwisho ya kufunga pazia la Ligi Kuu dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Zahera alisema moja ya mechi ambayo hataisahau ni ile ya raundi ya kwanza dhidi ya wekundu hao iliyomalizika kwa suluhu.

Alisema aliwaogopa Simba kwa sababu walikuwa wako moto wakitoka kufanya maandalizi mazuri ya msimu tofauti na wao walikuwa wamejiandaa kwa wiki mbili kutokana na hali ngumu ya klabu. “Tulikuwa tumetoka kucheza mechi nne na kushinda zote na mechi ya tano tulitarajia kucheza na Simba ambao walikuwa wako vizuri kwa hiyo nilipata hofu kwamba wangetufunga mabao matano au sita,” alisema. Alisema ni timu gani duniani inakwenda kucheza ligi ikiwa imejiandaa kwa wiki mbili kitu ambacho kilimpa hofu ya kufanya vibaya.

Pia, alisifu kikosi cha Azam FC kuwa kilikuwa bora. Zahera alisema utamu wa ligi ulipotea mapema kwani ilipendeza bingwa asingejulikana mapema mpaka michezo ya mwisho ingesaidia kujaza mashabiki wengi viwanjani na kuleta mvuto zaidi. Ukiachana na Zahera, wengine waliozungumzia ligi ni Kocha wa Azam, Abdul Mingange aliyesema hakuridhishwa na mwenendo mzima wa uendeshaji akisema ulikuwa mbovu.

“Tangu nimeanza kujihusisha kwenye mpira sijawahi kuona ligi mbovu namna hii kama msimu huu, timu nyingine ina mechi tano na nyingine 20, kwa hivyo hatuwezi kupata bingwa anayestahili,” alisema.

Kwa upande wake, Kocha wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji alisema ligi ya msimu huu ilikuwa ngumu, dunia nzima hajawahi kuona kwani timu tisa zilikuwa hazina uhakika baada ya kufanana pointi na kutofautiana kidogo. Haji ambaye alinusurika kushuka daraja baada ya kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Alliance hakuamini kama angebaki salama jambo lililomfanya kulia kwa furaha.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi