loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mliosoma Kiswahili changamkieni fursa, fundisheni ndani na nje

HIVI karibuni Rais John Magufuli alifanya ziara ya kikazi Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na kukitangaza vyema Kiswahili, kama njia ya kuhamasisha kitumike kufundishia kwenye nchi hizo katika ngazi ya shule ya msingi na sekondari.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli aliitangaza lugha hiyo kwa wakuu wa nchi hizo na kuonesha uzalendo wa aina yake, kwa sababu Kiswahili ni lugha yetu ya taifa yenye umuhimu kwa watu wengine pia wanaopaswa kujifunza na kukijua hasa kupitia sisi wenyewe.

Kwa ufupi, hiyo ni fursa ya ajira kwa Watanzania waliojifunza Kiswahili fasaha na Rais anachofanya ni jambo jema la kuwatafutia wananchi anaowaongoza ‘upenyo’ wa ajira.

Rais Magufuli amejaribu mara nyingi kuonesha kuwa Kiswahili kinawaunganisha wana wa Afrika hivyo kusisitizia kuwa ni cha muhimu zaidi.

Ninaunga mkono harakati hizo za Rais Magufuli ambazo kimsingi zinapaswa kuungwa mkono na Waafrika wote wanaofahamu thamani ya lugha ya Kiswahili.

Kadhalika, napenda kuwashauri Watanzania hasa waliojifunza Kiswahili kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika nchi mbalimbali zinazohitaji walimu wa lugha hiyo, kwamba wasiziache zikaenda kwa wengine kwa kuwa lugha hiyo asili yake ni nchini. Itakuwa vyema pia ikiwa Baraza la Kiswahili Tanzania litashiriki kuangalia fursa hizo kwa ajili ya Watanzania. Nina imani kuwa BAKITA iko vyema na imejipanga kwa hilo kwa sababu imeanza utaratibu wa kuwapata wenye sifa na kuwanoa hasa kwa kuwapa mbinu za kufundisha Kiswahili kwa wageni wasio kifahamu. Ujumbe wangu kwa Bakita ni kuhakikisha inawafundisha watu wengi zaidi mbinu hizo na ikiwezekana ijipenyeze katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuangalia Watanznaia wenye kuhitaji kunolewa ili nao wawanoe walio kwenye nchi hizo. Wakati tukichangamkia fursa tusijisahau Watanznaia kwa kuamini kuwa lugha hii ni yetu kutokana na ukweli kwamba asili yake ni nchini, tukijisahau tukabweteka wenzetu watatuacha mbali kwa sababu tayari imekwisha anza kufundisha kwenye vyuo vikuu nje ya Tanzania na wanaojifunza wapo makini kukipokea wakijua kitawanufaisha. Unaweza ukashangaa kuwa lugha imeanzia kwako lakini wanatokea waliotulia kujifunza mengi kuihusu na kukufanya ugeuke wa kufundishwa na wao. Kwa mtindo huo tutatimiza lengo? La hasha! Nawasihi wana Kiswahili kujibidiisha ‘kuzishika’ fursa na kuendelea kujifunza misamiati mipya kila inapobidi, ili Watanzania tubaki kuwa walimu bora wa Kiswahili. Hadi sasa walionolewa na Bakita ni 584 kati ya watu waliosajiliwa 727 ambapo kati yao wenye Shahada ni 632, wenye Shahada ya Uzamili ni 84 huku wenye Shahada ya Uzamivu wakiwa ni wanane. Pia, wenye Stashahada ya Uzamili ni watatu. Idadi hii inaweza kutuwezesha kama nchi kuwapeleka wataalamu nje ya nchi lakini bado kunahitajika kuwepo mkakati kabambe zaidi wa kuwapeleka nje ya nchi wataalamu wengi zaidi. Ninaamini kuwa fursa imekuja kwa wakati mzuri ambapo wengi wanahitaji ajira. Waliopelekwa vyuoni kujifunza Kiswahili hawana budi kufurahi kwa sababu ajira hizo zinawahusu. Nafahamu wapo waliokuwa wakijiuliza itakuwaje kwamba wamesoma Kiswahili katika dunia inayohitaji lugha nyingi zinazoonekana kuwa ngumu mfano Kifaransa, Kiingereza na nyinginezo, napenda kuwakumbusha kuwa kila jambo lina wakati wake na wakati wa wao kuchanua ndio huu

UZURI wa ngozi huanzia ndani. Hivyo unavyoitunza ngozi yako kwa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi