loader
Picha

Nchi za Kiafrika zilizosherehekea Eid al-Fitr leo

Baadhi ya nchi Barani Afrika zikiwemo Rwanda na Uganda zimesherehekea Sikukuu ya Eid al-Filtr leo, Jumanne.

Mbali na nchi hizo, Waislam katika nchi za Somalia, Ethiopia, Sierra Leone na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) nao wameshiriki ibada ya Eid baada ya kukamilisha mfungo wa Ramadhan.

Huko jijini Kigali, Sheikh Salim Hitimana amewaongoza Waislamu katika sala maalumu iliyofanyika katika viwanja vya Nyamirambo.

Kwenye sala hiyo Sheikh Hitimana amewasihi Waislamu kuendelea kutenda mema kama walivyokuwa wakifanya katika kipindi chote cha Ramadhan.

“Nautakia Umma wa Kiislamu Eid Mubaraka, nawanasihi waendelee na matendo ya upendo, kujikagua nafsi zao na kumcha Allah na kufanya kazi kwa bidii kama walivyofanya katika kipindi chote cha mfungo,” amesema.

Kutokana na nchi ya Saudi Arabia kuwa nchi yenye ushawishi mkubwa hasa linapokuja suala la muandamo wa mwenzi na kutangaza kuwa leo ni Sikukuu ya Eid, baadhi ya Waislamu watasherehekea leo sikukuu hiyo, japo mamlaka za nchi zao hazijatangaza Eid.

MAHOJIANO yenye lengo la kuamua mustakabali wa uwepo madarakani wa ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi