loader
Jay-Z atangazwa bilionea Na. 1 wa Hip Hop duniani

Jay-Z atangazwa bilionea Na. 1 wa Hip Hop duniani

Jarida maarufu duniani la Forbes limemtangaza mwanamziki wa Hip Hop kutoka Marekani Shawn Carter ‘Jay-Z’ kuwa ni rapa wa kwanza duniani kuingia katika orodha ya mabilionea.

Inaelezwa kuwa, mafanikio ya mwanamuziki huyo yamekuja baada ya kujenga utajiri wake kupitia kazi zake za kisanii, mitindo na uwekezaji kwa miaka kadhaa iliyopita.

Jarida hilo la Forbes limekadiria utajiri wake kuwa dola za Marekani bilioni 1/-, sawa na Shilingi trilioni 2.4/-.

Inaelezwa kuwa mume huyo wa mwimbaji Beyonce amefanikiwa kutokana na kujenga miradi yake na sio tu kuitangaza.

Hatahivyo Forbes imekanusha taarifa zilizokuwa zikiendelea kuwa Jay-Z na mtayarishaji Dr Dre walikuwa tayari wamefikia hadhi ya kuwa mabilionea kabla ya kutolewa kwa taarifa hii.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d25530981f73c51f98b3d723ef6a3423.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi