loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tamisemi imetekeleza vyema sera ya elimu

HIVI karibuni Wizara ya Nchi Ofi si ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ilitangaza kuwachukua wanafunzi wote wa kike wenye sifa za kujiunga na kidato cha tano na elimu ya ufundi.

Hilo ni tukio la kwanza kuwahi kutokea nchini ambapo wanafunzi 108,644 sawa na asilimia 98.31 ya wanafunzi 110,505 wenye sifa waliotangazwa kuchaguliwa mwaka huu kujiunga kidato cha tano wamepata nafasi hiyo.

Zamani wakati serikali ilipokuwa ikitangaza nafasi hizo, wanafunzi waliokuwa wakikosa nafasi hizo walikuwa wote, wa kike na kiume na kulazimika kungojea hadi chaguo la pili litokee.

Lakini kwa mwaka huu, wanafunzi wa kike wote wamechukuliwa katika chaguo la kwanza huku kati ya wanaongojea chaguo la pili wote wakiwa ni wanaume ambao idadi yao ni 1,861.

Ninapongeza utekelezaji kivitendo wa mikataba ya kimataifa inayolenga kumwinua mwanamke.

Lengo namba sita la malengo 18 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030 (SDG 2030) ni upatikanaji elimu bora kwa wasichana.

Tamisemi imetekeleza kivitendo malengo hayo ambapo hata sera ya elimu ya hapa nchini inasisitizia ubora wa elimu kwa wasichana.

Imetekeleza kwa kuanza na kuimarisha miundombinu ya masomo kwa kujenga mabweni mengi ya wasichana na sekondari nyingi katika mikoa mbalimbali nchini.

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi (Elimu), Tixon Nzunda alisema serikali imepeleka Sh bilioni 29 za ujenzi wa madarasa na mabweni mikoa mbalimbali nchini kuanzia Januari mwaka huu.

Mabweni na sekondari hizo ni mkombozi sahihi wa wasichana, lakini ukombozi huo ukamilike inapaswa wasichana hao kutoishia ngazi hiyo ya elimu bali waendelee hadi ngazi za vyuo vikuu.

Kutimiza hayo, jamii inapaswa kuunga mkono utekelezwaji sera ya kumwinua msichana kupata elimu.

Hapa nawaasa zaidi wazazi, walezi, walimu na jamii nzima kwa ujumla.

Lakini pia wanafunzi wenyewe wasijione kama hawahusiki kujipigania haki za za masomo.

Wao ndio askari wa kukabiliana na jambo linaloweza kuwasababishia kutofikia malengo.

Nitafurahi zaidi kusikia ongezeko la wasichana masomo ya sayansi ili watoe mchango mkubwa kwa maendeleo ya shughuli za kisayansi nchini.

Ushirikiano kati ya jamii na serikali utawezesha wanafunzi wa kike kumudu masomo ya sayansi.

Mfano mzuri matokeo ya mwaka huu wasichana 646 wamejiunga shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi (vipaji maalumu).

Idadi hiyo ni kutoka wanafunzi 1,462 ambapo wavulana 816 nao wamechaguliwa kujiunga.

Hivyo, wasichana mliochaguliwa kuingia kidato cha tano hampaswi kubweteka bali msome kwa umakini na kuheshimu maadili ya shule mfaulu.

Haitakuwa na maana kama mkiishia elimu ya ngazi ya kidato cha tano au sita kutokana na mimba, utovu wa nidhamu na mengine mabaya.

Itapendeza kama idadi hii ya mlioingia kidato cha tano ndio ikawa hiyo hiyo hadi vyuo vikuu.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: EVANCE NG’INGO

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi