loader
Picha

Esperance yaigomea CAF uamuzi wa kurudia mechi

Esperance Tunis ya Tunisia imekata rufaa kupinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) juu ya ulioipokonya timu hiyo taji la Klabu Bingwa Afrika na kuitaka irudiane na Wydad Casablanca ya Morocco.

Mechi ya pili iliyokuwa iamue bingwa wa michuano hiyo ilisitishwa baada ya Wydad kususia mechi wakipinga kukataliwa goli lao huku mwamuzi wa mchezo huo akishindwa kuthibitisha uhalali wake kwa kuwa mashine za VAR zilikuwa hazifanyi kazi.

Baada ya kususia huko, Esperance ilitangazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo yenye utajiri wa fedha kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Baada ya CAF kutengua ubingwa huo na kuitaka Esperance kurejesha Kombe na medali na kuamua kukata rufaa.

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi