loader
Picha

Muuguzi atupwa jela maisha kwa kuua wagonjwa 85

ALIYEKUWA muuguzi wa hospitali mbili tofauti nchini Ujerumani, Niels Hogel (42) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuua wagonjwa 85 kwa makusudi.

Jaji wa mahakama iliyomtia hatiani muuguzi huyo, Sebastian Buehrmann alimuelezea Högel kama mtu asiyezingatia maadili ya taaluma yake. Muuguzi huyo tayari anatumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuua wagonjwa wawili kwa kuwapa dawa iliyowaua wagonjwa wawili wa moyo, matukio yaliyotokea mwaka 1999 na mwaka 2005.

Jaji huyo alisema muuguzi huyo anaaminika kuwa muuaji hatari katika historia ya Ujerumani na kwamba amekuwa akifanya matukio hayo ya kikatili dhidi ya wagonjwa na baadhi akiwaua kwa makusudi na kudai atawafufua tena. Mmoja wa watu aliofanya kazi nao muuguzi huo, aliviambia vyombo vya habari kuwa walizoea kumuita Hogel Rambo kutokana na tabia yake ya ubabe.

Hata hivyo baada ya taarifa zake kufahamika, muuguzi huyo alikamatwa na kushtakiwa na kwamba siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi yake mahakamani aliomba msamaha kwa ndugu wa wagonjwa waliokufa kutokana na yeye kuwaua.

“Ninaomba msamaha kwa kila mmoja wenu kwa matendo niliyofanya kwa miaka yote hiyo,”alisema Hogel siku ya mwisho ya kutolewa hukumu yake.

Awali muuguzi huyo alituhumiwa kuwaua wagonjwa 100 kaskazini mwa mji wa Delmenhorst na Oldenburg. Hata hivyo, Polisi wanasema huenda idadi ya vifo ni kubwa zaidi ya hiyo na huenda kuna miili imetupwa au kuchimbiwa mahali na muuaji huyo. Awali Högel akiwa mahakamani alikiri kuua wagonjwa 55, katika mji wa Oldenburg.

KOREA Kusini imechukua hatua kudhibiti kusambaa virusi vya corona kufuatia ...

foto
Mwandishi: OLDENBURG, Ujerumani

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi