loader
Picha

Hoteli kuajiri watu 300 Arusha

HOTELI ya kisasa ya Gran Melia yenye vyumba 171 inatarajia kuanza kazi Julai mwaka huu na kutoa ajira kwa watu zaidi ya 300 jijini Arusha.

Hoteli hiyo yenye ghorofa tano, ipo katika eneo la Sabasaba ya zamani na ni hoteli ya kipekee kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza jana katika ukaguzi wa hoteli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema uwepo wa hoteli hiyo umechangia ukuaji wa ajira kwa Watanzania pamoja na sekta ya Utalii.

Alisema hoteli hiyo ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu itasaidia watu mbalimbali ikiwemo ukuaji wa sekta ya utalii, kwani Arusha ni Jiji la Utalii hivyo kutokana na uwepo wa watalii wengi kufika na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini watapata muda wa kulala katika hoteli hiyo ya kisasa zaidi.

Naye Mkurugenzi wa hoteli hiyo, Nicolas Koning alisema hoteli hiyo ni ya kisasa zaidi na imegharimu Sh bilioni 184 na ipo Zanzibar, Serengeti na Arusha.

Aliishukuru serikali kwa kuwekeza mazingira mazuri kwa wawekezaji ndio maana wameamua kufanya uwekezaji huo wa hoteli nchini Tanzania.

“Kwa kuanzia tumetoa ajira 200 kwa watanzania ambapo lengo letu ni kutoa ajira zaidi 300 katika hoteli hii hivyo tumewekeza kutokana na sera nzuri ya Rais, Dk John Magufuli katika masuala ya uwekezaji,” alisema.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimesema, mkoa wa Pwani una ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi