loader
Picha

Rwanda ya 1 EAC kuzalisha simu za kisasa

SIMU za mkononi zinazozalishwa nchini hapa na kiwanda cha Mara Corporation zitaanza kuuzwa katika masoko ya kitaifa na kimataifa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.

Kwa kuanza uzalishaji huo, Rwanda inakuwa nchi ya kwanza kuzalisha simu za kisasa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Awali, bilionea wa Tanzania, Dk Reginald Mengi aliyeaga dunia mwezi uliopita, alikuwa na ndoto za kuanzisha kiwanda cha simu za kisasa, kompyuta na vifaa vyake na pia kuuza nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya magari na mitambo mbalimbali.

Akizungumza jijini humu hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa Mara Corporation, Ashish Thakkar alisema ujenzi na kuweka tayari kiwanda katika Eneo Huru la Uwekezaji (EPZ) katika wilaya ya Gasabo uko katika hatua za mwisho.

Alisema kiwanda cha simu cha Mara Rwanda kitaajiri watu 200 kuanzia siku ya kwanza ,asilimia 16 ya wafanyakazi hao watakuwa wanawake wakiwa na mkakati wa maendeleo wa miaka 10. Simu hizo za thamani ya dola za Marekani 100 na dola 200, zinazotengenezwa nchini hapa zinatarajiwa kukuza huduma za dijiti pia mtandao wa intaneti kuenea Rwanda na Afrika Mashariki.

Alisema baadhi ya simu za mkononi zitakuwa kwa soko la Rwanda na nyingine kwa ajili ya soko la kimataifa katika bara la Afrika na sehemu nyingine duniani.

Thakkar alisema kutakuwa na nembo inayoonesha imetengenezwa Afrika na zitakazotengenezwa kwa soko la ndani zitakuwa na nembo mbili; zinazoonesha zimetengenezwa Rwanda na inayoonesha imetengenezwa Afrika.

Kiwanda cha Mara Corporation, pia kinamiliki Banque Populaire du Rwanda (BPR),inayotengeneza simu za mkononi Afrika Kusini kwa uwekezaji wa dola za Marekani milioni 100 walipoanza huduma mwaka 1996.

Nchi za Afrika Mashariki, kwa kiasi kikubwa zinategemea simu kutoka katika nchi za Ulaya na barani Asia, hususan China.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimesema, mkoa wa Pwani una ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi