loader
Picha

Timu za Uganda, Tanzania zatua Rwanda

TIMU za taifa za mchezo wa kikapu za Tanzania na Uganda za wanaume na wanawake zilitua jijini hapa Jumapili mchana tayari kwa mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 16.

Mashindano hayo yanatambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu, Fiba. Mashindano hayo yatakayofanyika kwa wiki nzima, pia yatatumika kwa ajili ya kufuzu kwa mashindano ya Afrika kwa umri huo, na yalitarajia kuanza jana Jumatatu na yatafanyika hadi Juni 15 kwenye Uwanja wa Amahoro. Hadi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, timu za Misri na Ethiopia zilikuwa hazijathibitisha kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza juzi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Rwanda (Ferwaba), Desire Mugwiza, alisema kuwa maandalizi yote yako vizuri tayari kwa mashindano yenye mafanikio.

Wakati wenyeji watakuwa wakipambana kusaka tiketi ya kushiriki mashindano ya U16 ya Afrika kwa wanaume, wasichana wao wenyewe tayari wamejihakikishia nafasi hiyo baada ya Rwanda kuwa wenyeji wa mashindano hayo ya Afrika yatakayofanyika mwezi Agosti.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi