loader
Picha

Rayon yashinda kwa penalti

TIMU ya AS Kigali imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Amani, lakini Rayon imesonga mbele kwa mikwaju ya penalti.

Katika mchezo wa kwanza Rayon Sports nayo ilishinda 1-0 na kufanya matokeo ya ujumla kuwa 1-1 baada ya AS Kigali kushinda mchezo wa pili na kufanya timu hizo kupigiana penalti ili mshindi apatikane na Rayon wakapata penalti 4-2.

Hata hivyo, pamoja na kufungwa kwa penalti, lakini AS Kigali nao wamesonga mbele kwa tiketi ya `best losers’ na timu zote hizo zimetinga hatua ya 16 bora na zinasubiri jua nani watacheza nao katika hiyo inayofuata.

Kiungo Janvier Benedata alifunga bao katika dakika ya 26 na kufanya mchezo huo kuongezewa muda wakati kipa wa AS Kigali Bate Shamiru akiwa kikwazo kwa wachezaji wa Rayon Sports Michael Sarpong, Gilbert Mugisha na Suleiman Mudeyi kupata mabao.

Hata hivyo, kipa huyo mzaliwa wa Uganda alikosa penalti wakati wa kupiga mikwaju hiyo, kabla wachezaji wa Rayon, Sarpong, Christophe Bukuru, Djabel Manishimwe na Prosper Donkor walimfunga kipa huyo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi