loader
Picha

Umeme Rufiji utakavyojenga uchumi

“TUNAMPONGEZA na kumuunga Rais John Magufuli mkono kwa juhudi zake za kuhakikisha mradi wa bwawa la umeme Rufiji (RHPP) unajengwa. Serikali zetu za Afrika zinatakiwa kuwekeza kwenye miradi kama hii kwani ni nguzo kubwa ya kuinua uchumi, kuchangia kukua pato la taifa, kuongeza ajira na kulinda mazingira.”

Hii ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka aliyotoa kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa dhamana za kibenki kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo wa umeme.

Katika ushirikiano wa kwanza wa kifedha, CRDB, UBA, zimeshirikiana na benki ya Afrieximbank na nyingine za Misri kutoa dhamana za kibenki kwa mradi huo wa RHPP ambao baada ya kukamilika, utazalisha megawati 2100 za umeme zitakazoongezwa kwenye gridi ya taifa.

Kukamilika kwa mradi kutafanya uwepo wa megawati maradufu ya zilizopo sasa na kusaidia kupunguza matatizo ya uhaba wa umeme pamoja na ukubwa wa bei.

Juni 2017 ndipo Rais John Magufuli aliagiza kuanza mchakato wa kuzalisha umeme kupitia mradi wa Rufuji ili kuwa na umeme wa uhakika.

Awali, mradi ulitathiminiwa mwaka 1980 kwamba unaweza kuzalisha umeme na kuongeza mara mbili ya unaozalishwa sasa.

Tayari historia imeandikwa baada ya Rais Magufuli kutiliana saini mkataba wa dola za Marekani bilioni 2.95 (takribani Sh trilioni 6.6 ) kwa mkataba baina ya Shirika la Umemem (Tanesco) na JV ya Arab Contractors/ Elsewedy Electric ya Misri .

Mkataba huo ni wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme wa gridi 2100 kwenye mradi huo wa Rufiji uliosubiriwa kwa zaidi ya miaka 40 .

Taasisi za kibenki zimeongeza nguvu ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuongeza uzalishaji wa umeme baada ya benki ya UBA Tanzania kwa kushirikiana na CRDB, benki ya Afreximbank kutoa dhamana ya fedha za awali.

Benki hizo zimetoa dola za Marekani milioni 516 sawa na takribani Sh trilioni 1.16 ambazo zinahitajika na JV ili kuweza kupata idhini ya serikali ya kuendesha mradi huu.

Hii ni sawa na asilimia 70 ya gharama ya mradi huu huku asilimia 30 iliyobaki ambao ni sawa na dola milioni 212 milioni (Sh bilioni 496) zikitolewa na benki za nchini.

Akizungumza wakati wa kutoa dhamana hiyo, Mkurugenzi wa Masuala ya umma na Fedha wa UBA Tanzania, Timothy alisema benki yake inaunga mkono mradi wa umeme wa Rufiji ambao ni moja ya njia sahihi ya kufikia nchi ya viwanda mwaka 2025, kukuza uchumi na hata kulinda mazingira.

“Kwa matarajio yetu, tunaamini ukuaji wa na upatikanaji wa uhakika wa umeme utachangia kupungua kwa bei yake kutokana na umeme unaozalisha kwa njia ya maji kuliko umeme wa gesi jua au hata wa upepo,” anasema na kusisitiza kuwa umeme wa maji pia utaepusha athari kwa mazingira .

Timothy anasema madhumuni ya benki UBA kwenye nchi zaidi ya 20 inapofanya biashara ni kuendeleza miradi ya miundombinu inayosaidia uchumi na kukuza ustawi wa maisha ya kila mwananchi kutokana na mradi huo wa umeme unaoandika historia kwa nchi.

Rais Magufuli aliwapongeza Arab Contractors & Elsewedy Electric ya Misri kwa kushinda zabuni ya kujenga mradi wa bwawa la umeme Rufiji (RHPP) wenye thamani ya dola bilioni 2.95 sawa na Sh trilioni 6.558. Wakandarasi hao wanatarajiwa kutumia miezi sita kwa hatua ya awali na miezi 36 kwa kukamilisha mradi wote na kuweka historia ya kumaliza mradi mkubwa kwa miezi 42.

Kwa sababu hiyo Benki ya UBA Tanzania na CRDB Bank Plc zilifikia makubaliano wa ushirikiano wa kihistoria wa kifedha kwa kutoa dhamana ya kibenki ya dola milioni 737.5 sawa na Sh trilioni 1.7.

Dhamana hiyo inahitajiwa katika umoja wa kampuni za Arab Contractors na Elsewedy za Misri kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bwawa la umeme Rufiji (RHPP) wenye thamani ya dola bilioni 2.95 sawa na Sh trilioni 6.558.

Mradi huo unatokana na mkataba uliotolewa kwa umoja huo na serikali ya Tanzania Desemba mwaka jana ili kuongeza umeme zaidi utakaofanikisha ndoto ya nchi ya kuwa taifa la uchumi wa viwanda.

Kwa mujibu wa masharti ya mkataba, umoja huo unatakiwa kutoa dhamana za benki za kigeni na ndani za dola milioni 737.5 zikiwa sehemu ya utekelezaji wa mradi na malipo ya awali ya mradi huo.

Mradi huu wa umeme wa Rufiji wa kuzalisha megawati 2,115, ni miongoni mwa miradi ya kimkakati ambao katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 umetengewa Sh trilioni 1.443.

Miradi mingine ya kimkakati ni wa kusambaza nishati vijijini na upanuzi wa mradi wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi I wa megawati 185. Miradi hiyo mitatu kwa pamoja itagharimu Sh1.86 trilioni.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti bungeni, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema bajeti ya mwaka ujao inalenga kutekeleza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu.

Afrika ni bara lililobarikiwa kuwa na maliasili nyingi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi