loader
Picha

Uganda yapania kumzuia Salah

KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Sebastien Desabre amesema kuwa atatumia ujuzi wake wote alionao kuhakikisha wanamzuia nyota wa Misri anayecheza soka England.

The Cranes iko katika Kundi A pamoja na wenyeji Misri katika mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, yatakayofanyika nchini humo kuanzia Juni 21 hadi Julai 9. Timu hiyo ya taifa ya Uganda imepangwa kukutana na Misri katika mchezo utakaofanyika Juni 30 jijini Cairo nchini humo.

Uganda, ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, mbali na wenyeji Misri ambao wametwaa taji hilo mara saba, wako pia na mabingwa mara mbili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR) na Zimbabwe.

Hata hivyo, kocha huyo wa The Cranes alisema kuwa sio kundi jepesi, lakini Uganda ina matumaini ya kusonga mbele katika mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanashirikisha timu 24.

Nahodha na kipa Denis Onyango na Faruku Miya ndio wachezaji wa Uganda wanaotajwa sana katika vyombo vya habari, huku wachezaji wa DRC Cedric Bakambu na Khama Billiat wa Zimbabwe nyota wengine wako katika orodha hiyo. Lakini kutoka Uganda, hadi Ulaya na kurudi tena Afrika, ni Mmisri Mohamed Salah ambaye amekuwa akitajwa kila mahali.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi