loader
Picha

Kiir awazia uraia watoto wake Kenya

RAIS Salva Kiir amesema anatamani watoto wake wapate pia uraia wa Kenya kwa kuwa walizaliwa nchini humo. Aidha, amesema anaichukulia Kenya kama nchi yake ya pili kutokana na kuwa nchi jirani na yenye uhusiano mwema na Sudan Kusini.

“Naichukulia Kenya kama makazi yangu mengine, ni nyumbani kabisa. Na mara nyingi nawafikiria watoto wangu. Wamezaliwa hapa (Kenya), hivyo nadhani wanastahili uraia wa Kenya,” alisema Rais Kiir wakati wa ibada ya kila mwaka ya kuliombea taifa la Kenya. Kiir alikuwa mwalikwa katika hafla hiyo.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa Sudan Kusini kuweka mbele maslahi ya taifa ili kuleta haki na usawa miongoni mwa raia wa nchi hiyo, hali itakayosaidia kuondoa misuguano isiyo ya lazima. “Uongozi haujalishi nani ni rais wa nchi, bali ni kuhudumia wananchi.

Watu wa Sudan Kusini wanahitaji sana amani ili wapate huduma bora, ndiyo maana kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania amani. Sisi kama Kenya tupo tayari kufanya kazi nawe na viongozi wengine ili kuhakikisha Sudan Kusini inakuwa na umoja wa kweli, umoja utakaozaa amani ya kudumu. Ndiyo ndoto yangu na hata ya viongozi wengine katika jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)…,” alisema Rais Kenyatta.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: JUBA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi