loader
Picha

Sudan Kusini kutumia bandari Dar

SERIKALI ya Tanzania imekubaliana na serikali ya Sudan Kusini kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usafirishaji ili nchi hiyo ipitishe mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, ushirikiano kati ya nchi hizo ulikuwepo tangu mwaka 2011 lakini sasa unaimarika zaidi.

“Itakumbukwa kwamba uhusiano kati ya Sudan Kusini na Tanzania ulianza tangu mwaka 2011 walipopata uhuru lakini sasa uhusiano huu unaimarika katika usafirishaji kwa kutumia bandari,”amesema Waziri Kabudi.

Amesema Februari mwaka huu serikali za nchi hizo zilikubaliana kushirikiana kielimu na kwamba, Tanzania imekubali kuisaidia Sudan Kusini kutengeneza vitabu vya Kiswahili, kuendelea kutoa mafunzo ya lugha hiyo, na kuwapa walimu wa kufundisha shule za msingi na sekondari.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, lengo la serikali ni kujenga bomba la mafuta kwenda Sudan Kusini ili kuifungulia nchi hiyo milango ya kibiashara.

"Kwa mwaka wanasafirisha tani 700,000 hadi 800,000 lakini sasa uhusiano huu unaimarika vizuri, hii ni kutokana na utendaji kazi kwa serikali hii ya awamu ya tano," amesema Kamwelwe.

“Sudan Kusini wameona waje Kusini mkataba ili mizigo yao yote ipite Dar es Salam, sasa tunaendelea na ukarabati wa usafiri wa reli na wa anga, jengo la tatu la abiria (TB III) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tumekabidhiwa kwa hiyo wafanyabiashara hawatapata taabu kuja kukagua mizigo yao ," amesema.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Sudan Kusini, Paul Mayom Akech amesema Tanzania ina historia kubwa na Sudan Kusini hivyo wataimarisha mkataba huo ili Tanzania iendelee kuwasaidia.

“Tumeonesha nia yetu ya kushirikiana na Tanzania na tuko tayari, tunaamini huu unaweza kuwa mwanzo mzuri kwetu kibiashara kwa sababu tuna fursa nyingi, tunaamini mtaendelea kutusaidia kama ambavyo mmekua mkitusaidia" amesema.

Waziri huyo pia ameiomba Tanzania kuingilia kati kusuluhisha uhusiano kati ya Khartoum na Juba kibiashara kwa kuwa si mzuri.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimesema, mkoa wa Pwani una ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi