loader
Picha

Stars yaongezewa makocha

BENCHI la ufundi la timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars limeongezewa nguvu kwa kupewa makocha wawili wa Misri.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana ilisema, makocha hao ni Abdelrahman Essa wa viungo na Ali Taha wa kutathmini kiwango.

“Assa na Taha wote ni raia wa Misri na tayari wamejiunga kwenye kambi ya Taifa Stars iliyopo Misri,” ilisomeka taarifa hiyo ya TFF iliyosainiwa na Ofisa habari wake Clifford Ndimbo.

Taarifa hiyo ilisema, makocha wote hao wamewahi kufanya kazi na kocha mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike. Benchi la ufundi sasa litakuwa na makocha wanne, mwingine ni kocha msaidizi, Hemed Morocco. Stars tayari ipo Misri kujiandaa na michuano hiyo iliyofuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Kesho inatarajia kucheza mechi ya kujipima nguvu na wenyeji Misri. Imepangwa kundi moja na Algeria, Kenya na Senegal na itaanza kurusha kete yake ya kwanza Juni 23 dhidi ya Senegal.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi