loader
Picha

Tamasha Kubwa Kuliko Yanga laiva

KAMATI ya kuhamasisha uchangiaji Yanga imesema maandalizi kuelekea tamasha lao la kubwa kuliko Jumamosi yameiva na kuhimiza Wanayanga kufanya mchakato wa manunuzi ya tiketi mapema.

Wakizungumza jana Dar es Salaam baadhi ya viongozi wa Kamati hiyo walisema tiketi zimeanza kuuzwa klabuni Yanga, Dar Live, Total Petrol Azikiwe Posta, Vunjabei Sinza, Robi One Kinondoni na sehemu mbalimbali ikiwemo mitandaoni.

Mmoja wa wajumbe hao, Saady Khimji alisema mambo yameshaiva hivyo ni wakati kwa wanayanga kujumuika pamoja kwenye tamasha hilo kuchangia timu hiyo kufikia malengo ya muda mfupi, ya kati na muda mrefu.

“Tunahimiza Wanayanga popote pale waliopo kujitokeza kwa wingi kuchangia kwani ni jambo kubwa na la kipekee,” alisema na kuongeza kuwa anatarajia baada ya tukio hilo kubwa kutakuwa na Yanga mpya. Kwa upande wake, Mjumbe Said Mrisho alisema tiketi zinauzwa kuanzia Sh 50,000 kwa kiwango cha chini, meza watu 10 kwa Sh milioni 10, VIP watu 10 kwa Sh milioni tano, VIM one Sh milioni moja kwa watu 10, VIM two Sh 100,000 kwa mtu mmoja.

Alisema tamasha hilo litakwenda sambamba na uuzwaji wa jezi inayouzwa Sh 35,000, lengo ni kukusanya pia fedha. Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema washiriki wanahimizwa kuvaa jezi za klabu hiyo siku hiyo na kwamba watu watakaonunua tiketi pia, watapendekeza rangi ya mapambo katika meza zao.

Alisema kwa watu ambao hawatapata fursa ya kutizama ‘Live’ kupitia televisheni na walioko nje ya nchi wanaweza kujiunga kupitia Pay Per View. Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya maandalizi, Dk Ruhago David alisema tamasha hilo lengo lake ni kukusanya Sh bilioni 1.5 zitakazosaidia katika mipango ya klabu hiyo kwenye usajili ukiwa ni mpango wa muda mfupi huku Katibu wake Deo Muta akisema wanayoyafanya sasa ni muendelezo wa yale waliyofanya Dodoma.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi