loader
Picha

Ndayiragije kutambulishwa Azam leo

BAADA ya kuachana KMC hivi karibuni, Kocha Ettiene Ndayiragije anatarajiwa kusaini mkataba na kutambulishwa leo na mwajiri wake mpya Azam FC. Baada ya utambulisho huo kocha huyo atatangaza rasmi majembe yake atakayofanya nayo kazi msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jana Meneja wa Azam FC, Philipo Alando alisema utambulisho wa kocha huyo utakuwa na maana kuwa anaanza kazi iliyopo mbele yake ya usajili wa wachezaji wapya anaowahitaji kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. “Kocha tumeshamalizana naye na kesho saa tano (leo) atasaini mkataba na kuanza kazi ya usajili kujiandaa na michuano iliyoko mbele yetu, tunawakaribisha waandishi wa habari kwa wingi, mje msikie mipango yake ijayo,” alisema.

Kwa sasa ni msimu wa usajili na klabu hiyo haijasaini mchezaji yeyote mpya zaidi ya kuwaongezea mkataba baadhi ya wachezaji wake wakiwemo Donald Ngoma, Yakubu Mohamed na Daniel Amoah, ikimsubiri kocha huyo ili kupendekeza kulingana na mfumo wake. Kibarua cha kwanza cha kocha huyo ni kuhakikisha anafanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa kutimua vumbi mwezi ujao.

Azam FC kama bingwa mtetezi wa michuano hiyo ilithibitisha kushiriki huku wengine walioalikwa kama Simba na Yanga zikijitoa kutokana na sababu mbalimbali. Mbali na michuano hiyo, timu hiyo msimu ujao inatarajiwa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na KMC, hivyo huenda ushiriki wao kwenye Kagame ukatumika kusaka wachezaji wapya kutoka kwa washiriki mbalimbali.

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi